Aliyekua beki wa klabu ya Barcelona Hector Bellerin ameondoka ndani ya klabu hiyo na kujiunga na miamba ya soka nchini Ureno klabu ya Sporting Lisbon.
Mchezaji Hector Bellerin ambaye alijiunga na klabu ya Barcelona akitokea klabu ya Arsenal ambayo ilimnunua mchezaji huyo kutoka timu ya vijana ya Barcelona mwaka 2011, Ambapo mchezaji huyo aligeuka kua mchezaji muhimu ndani ya klabu ya Arsenal.
Beki huyo mwenye miaka 27 sasa anayesifika kwa kasi ameondoka ndani ya klabu ya Barcelona kwa uhamisho huru akielekea klabu ya Sporting Lisbon. Mchezaji huyo amekua kwenye wakati mgumu ndani ya Barca kwani amefanikiwa kucheza michezo saba tu mpaka anaondoka klabuni hapo.
Beki huyo wa kulia anaonekana kuathiriwa zaidi na majeraha aliyokua anayapata ndani ya klabu ya Arsenal kwani alikua moja ya wachezaji muhimu sana ndani ya klabu ya Arsenal, Lakini ghafla amegeuka kua mchezaji asiekua na ubora mkubwa tena kutokana na majeraha aliyokua akiyapata.
Hector Bellerin amejiunga na Sporting Lisbon ili kwenda kuziba pengo la aliyekua beki wa kulia klabuni hapo Pedro Porro ambaye ametimkia klabu ya Tottenham Hotspurs ya nchini Uingereza, Hivo beki huyo wa kimataifa wa Hispania ndio atakua na jukumu la kuvaa viatu vya Porro.

