Inzaghi: Ilipaswa Tushinde kwa Namna Yeyote

Kocha wa klabu ya Inter Milan Simeone Inzaghi anasema ilikua lazima kushinda mchezo wao wa Robo fainali ya kombe la Coppa Italia dhidi ya Atalanta kwani wanahitaji kucheza fainali ya michuano hiyo.

Klabu ya Inter Milan ambayo haikua kwenye kiwango bora siku za karibuni kutokana na kutopata matokeo ya kuridhisha, Lakini jana ilifanikiwa kupata matokeo ya ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya klabu iliyokua kwenye kiwango bora klabu ya Atalanta.inzaghiKlabu ya Inter Milan chini ya kocha Simeone Inzaghi walifanikiwa kubeba taji la kwanza msimu huu la Supercoppa Italiana wakiwagaragaza wapinzani wao wakuu klabu ya Ac Milan katika fainali iliyopigwa nchini Saudia Arabia, Hivo klabu hiyo imebakiza hatua moja kuweza kufika fainali na kuwania taji la pili msimu huu.

Kocha Inzaghi anasema ni furaha kwao kushinda dhidi ya klabu bora kama Atalanta, Lakini pia akieleza kua wana furaha kwakua klabu pekee nchini Italia ambayo inashiriki kwenye michuano yote msimu huu ndani ya nchi hiyo.inzaghiSimeone Inzaghi pia amesema kua walicheza na klabu ya Atalanta huku wakiwa wanahitaji ushindi kwa gharama yeyote na walifanikiwa kushinda mchezo huo, Lakini akigusia ligi kuu ya Italia Serie A na kusema kua ingekua sio kiwango cha ajabu cha Napoli basi wangekua wanaongoza usukani wa ligi hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.