Maddison Aingia Kwenye Mawindo ya Man City

Kiungo wa klabu ya Leicester City James Maddison ameingia kwenye mawindo ya klabu ya Manchester City kuelekea dirisha kubwa la majira ya joto.

Kiungo James Maddison amekua kwenye kiwango bora ndani ya klabu yake ya Leicester Ciy kwa misimu kadhaa sasa, Hivo kuvifanya vilabu mbalimbali ndani ya ligi kuu ya Uingereza kuhitaji kupata saini ya kiungo huyo wa kimataifa  wa Uingereza.MaddisonKiungo huyo fundi mwezi Juni mwaka huu atakua anaingia mwaka wake wa mwisho kwenye mkataba wake, Hivo klabu ya Manchester City inawinda saini yake kwani inaelewa fika kua klabu yake lazima imuuze ili kuepuka mchezaji huyo kuja kuondoka bure hapo baadae.

Kiungo James Maddison tayari ameshafunga mabao saba kwenye ligi kuu ya Uingereza huku akionesha kiwango bora sana ndani ya Leicester City, Ikiwa ndo sababu kubwa ya mchezaji huyo kuhitaji ndani ya klabu ya Manchester City chini ya kocha Pep Guardiola.MaddisonTaarifa pia zinaeleza kiungo James Maddison anaweza kwenda kuvaa viatu vya kiungo wa kireno Bernardo Silva ambae inaelezwa ameomba kuondoka klabuni hapo, Hivo mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Uingereza wanaona kama mchezaji huyo ndo anaweza kufaa ndani ya timu hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.