Manchester United Yamvizia Kolo Muani

Klabu ya Manchester United ipo kwenye mpango wa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Kolo Muani anaekupiga klabu ya Eintrach Frankfurt inayoshiriki ligi kuu nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga.

Klabu ya Manchester United kwasasa imekua ikipata changamoto kubwa katika safu ya ushambuliaji wakikosa washambuliaji wa kiwango cha dunia, Kutokana na hali hiyo klabu hiyo imeamua kuingia sokoni na kutafuta mshambuliaji mwenye kiwango cha dunia.manchester unitedKolo Muani mshambuliaji ambaye anafanya vizuri kunako ligi kuu ya Ujerumani na klabu ya Eintracht Frankfurt vilevile akikumbukwa kwa kiwango kizuri alichoakionesha kwenye michuano ya kombe la dunia 2022 Qatar akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa.

Manchester United mpaka sasa wana washambuliaji wawili asilia kwenye kikosi ambao ni Wout Weghorst na Anthony Martial ambaye amekua akiandamwa na majeraha mara kwa mara, Huku Weghorst akiwa klabuni hapo kwa mkopo hivo watahitaji kupata mshambuliaji mwenye ubora mkubwa.manchester unitedKlabu ya Manchester United wanahitaji sana mshambuliaji wa kiwango cha dunia na ndio sababu klabu hiyo imekua ikihusishwa na washambuliaji wengi wenye ubora mkubwa sokoni kama Victor Osimhen, Harry Kane, pamoja na Kolo Muani ambaye inaelezwa United wameandaa kitita kizito ili kunasa saini yake.

Acha ujumbe