Meneja wa Leeds United, Marcelo Bielsa huwenda akafungashiwa vilago ndani ya viunga vya Elland Road baada ya muendelezo wa matokeo mabovu, baada ya kuchapwa 4-0 na Tottenham hapo jana.

 

bielsa, Marcelo Bielsa Akalia Kuti Kavu Leeds United., Meridianbet

Bielsa alijiunga na Leeds mwaka wa 2018 na kuiwezesha timu hiyo kurejea Ligi Kuu baada ya kukosekana kwa miaka 16 na kufanikiwa kushika nafasi ya tisa katika ligi msimu wa 2020/21.

Miaka miwili baadaye, Leeds iko alama mbili nyuma katika nafasi ya kushuka daraja baada ya kufungwa mara tano katika mechi zao sita walizocheza hivi karibuni.

Leeds wameruhusu mabao 21 katika michezo sita huku wakifunga mabao matano pekee, wakionyesha kuwa na safu ya ulinzi mbovu zaidi EPL msimu huu, wakiwa wamefungwa mabao 60 katika mechi 26, tano zaidi ya timu ya inayoshika mkia, Norwich.

Matokeo ya Leeds katika mechi 6 zilizopita:

January 22 – Leeds 0-1 Newcastle
February 9 – Aston Villa 3-3 Leeds
February 12 – Everton 3-0 Leeds
February 20 – Leeds 2-4 Man Utd
February 23 – Liverpool 6-0 Leeds
February 26 – Leeds 0-4 Tottenham

Meneja wa zamani wa Borussia Dortmund, Jesse Marsch anatajwa kama mrithi wa Marcelo Bielsa katika dimba la Elland Road endapo atafutwa kazi ndani ya timu hiyo.


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa