Lisandro Martinez amekuwa akilaumiwa kwa urefu wake na vyombo vya habari katika wiki za hivi karibuni, lakini anapolinganishwa uchezaji wake wa mipira ya angani dhidi ya Southampton na mabeki wa Chelsea, matokeo yake ni ya kushangaza.

Beki mpya wa kati wa Manchester United alisajiliwa kutoka Ajax akiwa na urefu wa futi 5’9 tu, na wachambuzi kama vile Jamie Carragher wametoa madai makubwa dhidi ya uwezo wake wa kucheza kwenye Ligi kuu.

Baada ya timu nzima kupata matatizo katika mechi mbili za ufunguzi wa msimu, Martinez alionekana kukosolewa vibaya na kila mtu.
Tangu wakati huo, amebadilika na kuwa mchezaji Bora wa Mechi mara mbili dhidi ya Liverpool na Southampton.
Muargentina huyo pia anaonekana kama atapokea Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Agosti wa klabu hiyo baada ya uchezaji wake.

Ukali wake, uwezo wake kwenye mpira na akili ni sifa tatu muhimu juu ya mchezaji huyo.
Walakini, kuna mambo mengi zaidi ambayo yanaleta mjadala mezani, ni pamoja na uwezo wake wa kucheza mipira ya kichwa, licha ya urefu wake, lakini Martinez ni mchokozi na jinsi anavyoruka kugombea mipira ya angani kunamaanisha kuwa si mzembe angani licha ya kimo chake.
Hilo limesisitizwa katika ulinganisho wa hivi majuzi.
Katika ushindi wa United dhidi ya Southampton, ambapo Martinez aliisaidia timu yake kubaki bila goli, beki huyo wa kati wa upande wa kushoto alishinda mipira ya angani mara tano kwa mujibu wa StatmanDave.

