Jean-Philippe Mateta ameibua mjadala mkubwa ndani ya Selhurst Park baada ya kuifahamisha Crystal Palace nia yake ya kuondoka katika dirisha la usajili la Januari. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa, mwenye umri wa miaka 28, anatazamwa kwa jicho kali na vigogo wa Ulaya, Aston Villa na Juventus, jambo linaloashiria kuwa safari yake na Palace huenda ikafika ukingoni mapema kuliko ilivyotarajiwa.
Licha ya taarifa hiyo, Palace hawako kwenye mpango wa kumuuza. Mateta bado ana mkataba hadi majira ya kiangazi 2027, na uongozi wa klabu umeweka msimamo kuwa ni dau nono pekee litakalowashawishi kuachana na straika wao tegemezi. Kwa sasa, milango haijafungwa kabisa, lakini pia haijafunguliwa kwa haraka, mpira bado uko katikati.
Kwa upande mwingine, Palace wana malengo makubwa msimu huu. Wanataka kuimarisha kikosi, kushindania taji la Conference League na kupanda nafasi za juu zaidi kwenye Ligi Kuu England. Tayari wamepata pigo la kuondoka kwa nahodha Marc Guehi aliyeuzwa Man City kwa pauni milioni 20, huku kocha Oliver Glasner akithibitisha ataondoka mwishoni mwa msimu.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Aston Villa wanaongeza kasi katika soko la washambuliaji, wakimfuatilia pia Tammy Abraham, lakini jina la Mateta bado lipo mezani. Nao Juventus hawajakata tamaa, ingawa sambamba na hilo wanafanya kazi ya kumsajili Youssef En Nesyri wa Fenerbahce kama mpango mbadala.
Kwa takwimu zake pale Palace, Mateta ana mabao 48 kwenye mechi 149, na mchango mkubwa katika ushindi wa FA Cup na Community Shield mwaka 2025 pale Wembley. Nje ya klabu, tayari ameonja ladha ya timu ya taifa ya Ufaransa kwa kufunga mabao mawili katika mechi tatu, na ndoto yake kubwa ni kuwa sehemu ya kikosi cha Kombe la Dunia.