Mbappe Aomba Msamaha Ufaransa.

 

Mshambuliaji wa Paris Saint-Germain na France, Kylian Mbappe amewaomba msamaha mashabiki wa Ufaransa baada ya timu hiyo kutolewa katika hatua ya 16 bora ya michuan na EURO 2020 baada ya kukosa penati.

 

“Ni ngumu sana kuufunika ukurasa huu. Huzuni kubwa na masikitiko baada ya kutolewa, tumeshindwa kufikisha malengo yetu,” alisema Mbappe
“Ninawaomba radhi kwa penalti ile. Nilitaka kuisaidia timu, lakini nimeshindwa. Sitaweza kupata usingizi, lakini hivi ndivyo ilivyo kwenye mchezo huu ninaoupenda zaidi.
“Nafahamu mashabiki wamehuzunika, lakini bado nawashukuru kwa sapoti yenu na kuendelea kutuamini.
“Kitu muhimu naamini tutarudi kwa nguvu kubwa kwenye michuano ijayo. Hongera na kila raheri Uswisi.” aliongeza Mbappe.

KUSANYA PESA HAPA!

IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!Meridianbet

INGIA MCHEZONI

Acha ujumbe