Wakati dirisha la usajili likiwa linaendelea, baadhi ya vilabu vinaendelea na mchakato wa kupata makocha wapya. EPL kunogeshwa na ujio wa Rafa Benitez.
Ni suala la muda tu kabla ya klabu ya Everton kumtangaza rasmi Rafa Benitez kama kocha mkuu wa klabu hiyo kuanzia msimu ujao wa EPL – 2021/22.
Benitez anatua Everton baada ya kuwa nje ya uwanja tangu alipotoka China na anahistoria ngumu na klabu hii ambayo ni mahasimu wakubwa wa Liverpool. Mashabiki wa Everton wanahisia kinzani kuhusu Benitez huku wengine wakienda mbali zaidi kwa kutoa vitisho vikali dhidi ya kocha huyu.

Upande wa pili, Nuno Espirito Santo ananukia Tottenham Hot Spurs. Nuno aliondoka Wolves na sasa anahusishwa na klabu hii ya London kuelekea msimu ujao. Nuno ataweza kuvaa viatu vya Mourinho? Atafanikiwa kumbakiza Harry Kane? Ni suala la muda tu.

Crystal Palace pia ipo mbioni kumrudisha Patrick Viera. Viera anarudi kwenye EPL sio kama mchezaji lakini anakwenda kuchukua mikoba ya Roy Hodgson ambaye ameamua kuchana na soka baada ya kujihusisha na mchezo huo kwa muda mrefu. Hakika msimu ujao utanoga zaidi!
IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!

