Manara : Tunaenda Kuchukua Ubingwa Mbele ya Yanga.

 

TUMEJIPANGA! Ndiyo kauli ya mkuu wa Idara ya Habari ya Simba, Haji Manara kuelekea mchezo wa Jumamosi dhidi ya Yanga.

Simba na Yanga wanashuka katika dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambao ulihairishwa Mei 8 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Manara amesema kuwa wameandaa mikakati mizuri ya kuhakikisha wanatwaa ubingwa mbele ya Yanga kwa mara ya nne mfululizo na kuweka rekodi.

 

“Mwenyekiti wa bodi, menejimenti ya Simba chini ya (CEO) wetu Barbara Gonzales lengo letu ni kupata matokeo uwanjani tu” amesema

Aidha Manara amesema kuwa wanaenda kwenye mchezo mkubwa ambao kutokana na rekodi ya timu hizo mbili ila lengo lao kubwa ni kuchukua ubingwa wa nne mfululizo.

“Tunaenda kuchukua ubingwa wa nne mfululizo na si hivyo tu bali bado misimu sita ijayo kutokana na jinsi tulivyojiandaa” amesema Manara.

Katika mchezo huo ambao endapo Simba itashinda itatangazwa kuwa mabingwa Manara alisema kuwa mechi hiyo ni ya heshima kwao kuweka rekodi hiyo mbele ya watani zao wa jadi.,

“Suala la ubingwa lilishatokea nakumbuka mwaka 1985 ambapo Simba ilikuwa ikihitaji ushindi na kutangazwa kuwa mabingwa ila mchezo ulivunjika dakika ya tano baada ya kutokea utata wa penalti na chama cha soka kwa wakati huo (FAT) kikawapa ubingwa Yanga” aliongeza

Aidha Haji ameomba (TFF) kuleta Kombe uwanjani kwa kuwa ndio siku ambayo watatangaza ubingwa mbele ya watani.

“Nchi za wenzetu ikitokea hali kama hii ya ushindi kwa timu inakuwa bingwa basi mamlaka husika zinakuja na kombe hivyo nawasihi TFF kufanya hivyo” alisema Manara


KUSANYA PESA HAPA!

IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!Meridianbet

INGIA MCHEZONI

Acha ujumbe