Patson Daka Atua Leicester City Kwa Dau La £23M

Mzambia aliyekuwa anacheza katika timu ya Salzburg ya nchini Austria, Patson Daka amefanikiwa kutua katika timu ya Leicester City ya nchini Uingereza tayari kusakata kabumbu pale Uingereza akiwa na uzi wa the Foxes!

Mchezaji huyo ana miaka 22 tu lakini tayari amefikia mafanikio makubwa sana huku akiwa na damu ya Zambia. Daka alianza kucheza soka mwaka 2014 akichezea Kafue Celtic huko Zambia.

Mwaka 2015, Daka alicheza mchezo wa kwanza akiwa na timu ya Taifa ya Zambia na mwaka 2017 alifanikiwa kushinda goli lake la kwanza akiwa katika jezi ya timu ya Zambia kabla ya kushinda tuzo ya mchezaji wa mwaka wa CAF kijana.

Daka akiwa na Clatous Chama wakati wa majukumu ya timu ya Zambia

Patson alijiunga na Red Bull Salzburg ya Austria ambapo aliisaidia kushinda taji la Austria Bundesliga akiwa na mwaka mmoja tu katika jezi ya Salzburg, hiyo ilikuwa ni mwaka 2018.

Akiwa na Salzburg Patson amefanikiwa kucheza kombe la ligi ya mabingwa ulaya, kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Austrian Bundesliga, huku akimaliza msimu wa 2020/2021 akiwa kama mfungaji bora wa ligi hiyo ya Austria.

Baada ya kutangazwa, Patson alieleza kuwa anafurahia sana kusajiliwa katika klabu hiyo ambayo amekuwa akiifuatilia toka ichukue ubingwa wa EPL mwaka wa kwanza katika ligi ya Uingereza EPL.


KUSANYA PESA HAPA!

IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!Meridianbet

INGIA MCHEZONI

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.