Golikipa wa zamani wa klabu ya Aston Villa na timu ya taifa ya Marekani Brad Friedel anaamini staa wa PSG Lionel Messi atatikisa zaidi ya Pele akihamia ligi kuu nchini Marekani.
Ikumbukwe gwiji wa timu ya taifa ya Brazil ndio mchezaji aliewahi kutikisa zaidi alipohamia nchini Marekani katika klabu ya New york Cosmos kwenye miaka ya 1975. Lakini golikipa huyo wa zamani wa Aston Villa amesema anaamini Messi atavunja rekodi hiyo.
Watu wengi wanaamini Messi atamalizia soka nchini Marekani na inaaminika klabu inayomilikiwa na David Beckham Inter Miami ilifanya jaribio la kumsajili staa huyo kutoka klabu ya PSG lakini ikashindikana.
David Beckham ambae alijiunga na klabu ya Los Angeles Galaxy mwaka 2007 na kuwavutia zadi mastaa wa kizazi chake kama Thiery Henry, Andrea Pirlo, Kaka, Frank Lampard, pamoja Steven Gerrard.
Inaaminika zaidi kua Messi kabla ya kustaafu soka atakwenda kushiriki ligi kuu ya Marekani na Freidel anaamini itakua jambo kubwa na lenye mapokezi zaidi kuliko Pele, Ambaye alikua na mapokezi makubwa zaidi kwenye historia ya ligi hiyo.

