Mkurugenzi Man United Kujiuzulu

Taarifa mbalimbali kutoka ndani ya klabu ya Man United zinaeleza kua mkurugenzi mkuu wa klabu hiyo Richard Arnold huenda akajiuzulu majukumu yake ndani ya timu hiyo kutokana na sakata la Mason Greenwood.

Mkurugenzi Richard Arnold yupo kwenye presha ya kujiuzulu ndani ya Man United kutokana na ishu ya mshambuliaji wa klabu hiyo Mason Greenwood, Kwani inaonekana Mkurugenzi huyo ameshindwa kusimamia sakata la mchezaji huyo vizuri.Jana klabu ya Manchester United walitoa taarifa kwa umma juu ya kuachana na mshambuliaji Mason Greenwood baada ya kujadiliana kwa kina juu ya mustakabali wa mchezaji huyo siku za usoni kitu ambacho kimemuekea doa bosi huyo.

Bosi Richarld Arnold anaonekana kama amefeli kwa namna katika kuhakikisha analimaliza vizuri suala la Mason Greenwood, Hivo watu wengi wakiamini jambo hilo limefika katika hatua hiyo kutokana na bosi huyo kushindwa kulisimamia vizuri.man unitedTaarifa hizi kama zitathibitishwa siku za usoni ni wazi kua klabu ya Man United itakua imebadilisha Wakurugenzi wakuu wawili tayari ndani ya miaka miwli, Kwani Arnold hana miaka miwili ndani ya klabu hiyo tangu achukue mikoba ya Ed Woodward.

 

Acha ujumbe