Man United Wapiga Chini Ofa ya West Ham kwa Maguire

Klabu ya Man United wanatajwa kupiga chini ofa ya klabu ya West Ham kwajili ya beki wake raia wa kimataifa wa Uingereza Harry Maguire.

West Ham wanaelezwa kua walituma kiasi cha paundi milioni 20 ambapo klabu ya Man United wameona kiwango hicho sio thamani halisi ya beki huyo ambaye walimnunua kwa paundi milioni 80 na kua beki ghali zaidi duniani miaka minne iliyopita.Man unitedHarry Maguire amewekwa sokoni kwakua hayupo kwenye mipango ya kocha Erik Ten Hag na klabu hiyo wanahitaji kiwango cha pesa ambacho wanaona kitaendana na thamani ya beki hiyo na sio kiwango ambacho wamekitoa West Ham.

Klabu ya Man United wanaelezwa kua wanatizamia zaidi kuuza wachezaji kadhaa ili kuweza kupata pesa zaidi kwenye usajili ambao wanaendelea kuufanya, Hivo wanahitaji viwango vizuri vya pesa kwa wachezaji ambao wanawauza.Man unitedMaguire kwa upande wake anaamini bado anaweza kupambania nafasi ndani ya klabu hiyo, Lakini klabu hiyo haipo tayari kuendelea nae msimu ujao na ndio maana wamemueka sokoni hivo West Ham wanatakiwa kupandisha dau kama wana nia na mchezaji huyo kwelikweli.

Acha ujumbe