Klabu ya Man United imemrudisha aliyekua beki wake Jonny Evans kwa mkataba wa muda mfupi beki huyo ambaye alikua anaitumikia klabu ya Leicester City ambayo imeshuka daraja msimu uliomalizika.
Jonny Evans inaelezwa amesaini mkataba wa muda mfupi na klabu hiyo ambao utamuwezesha kutumika ndani ya kikosi cha Man United katika micheza ya maandalizi ya msimu ambapo anatarajiwa kusafiri na timu pia kuelekea maandalizi hayo ya msimu.
Jonny Evans amesaini mkataba wa muda mfupi na Mashetani wekundu lakini mpaka sasa haijafahamika ni muda gani beki huyo atakua ndani ya klabu hiyo, Hivo mpaka sasa haijafahamika muda ambao atakua ndani ya klabu hiyo.
Taarifa mbalimbali zinaeleza huenda beki huyo akawa amejumuishwa kwenye kikosi cha Man United kwajili ya kuangaliwa uwezo wake na kama atamshawishi kocha Ten Hag basi anaweza kubakizwa kwajili kutumika ndani ya klabu hiyo.
Baada ya David De Gea kuondoka klabuni hapo Man United ilikua inakosa mchezaji ambaye amewahi kushinda taji la ligi kuu ya Uingereza, Lakini baada ya Jonny Evans kujumuisha kwenye kikosi hicho anakua mchezaji pekee mwenye medali ya ligi kuu ya Uingereza.

