Sanamu la Wenger Lazinduliwa Emirates

Kocha wa zamani wa Arsenal mwenye heshima kubwa sana ndani ya klabu hiyo Arsene Wenger amefanikiwa kupewa heshima anayostahili klabuni hapo baada ya kuzinduliwa kwa sanamu lake leo.

Kocha Wenger ndio kocha ambae amefanikiwa kuwapa mafanikio makubwa klabu hiyo kutoka kaskazini mwa jiji London, Kwani amefanikiwa kuwapa mataji tofauti tofauti ikiwemo mataji manne ya ligi kuu ya Uingereza.wengerMapema leo nje ya uwanja wa Emirates wamezindua sanamu lenye picha ya kocha huyo wa kimataifa wa Ufaransa ambae kwasasa anafanya kazi katika shirikisho la soka ulimwenguni FIFA akiwa moja ya makocha wenye heshima kubwa katika soka la Uingereza.

Kocha huyo amepewa heshima hiyo kubwa ambayo hakuna mda yeyote wa soka  ambaye anaweza kupinga heshima aliyopewa kocha huyo, Kwani Mfaransa huyo ndio kocha ambaye ameiongoza klabu hiyo kwa michezo mingi na pia akifanikiwa kushinda michezo mingi.wengerKocha Wenger amepewa heshima hiyo leo ikiwa ni muda mchache umepita baada ya kutajwa katika orodha ya makocha wenye heshima wa muda wote ndani ya Uingereza katika tuzo maalumu zinazofahamika kama Premier League Hall Of Fame.

Acha ujumbe