Kiungo wa klabu ya Manchester United Fred Rodrigues raia wa kimataifa wa Brazil anatajwa anakaribia kujiunga na klabu ya Galatasaray ya nchini Uturuki ambao ni mabingwa nchini humo.

Fred amekua kwenye mazungumzo na klabu ya Galatasaray kwa wiki kadhaa sasa na wanatajwa kufikia makubaliano, Huku kinachosubiriwa kwa kiungo ni mabingwa hao wa soka kutoka nchini Uturuki kutuma ofa kwa klabu ya Man United.FredKlabu ya Galatasaray baada ya kukubaliana maslahi binafsi Fred sasa wanatajwa kuandaa ofa na kuituma klabu ya Manchester United kwajili ya kuhakikisha dili hilo linakamilika mapema ili wasikumbane na vikwazo kwa timu zingine.

Klabu kadhaa zilikua zinahitaji huduma ya kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil ikiwemo klabu ya Fulham ya nchini Ungereza vilivile vilabu kutoka nchini Saudia Arabia hivo Galatasaray wanataka kuhakikisha wanakamilisha dili hilo haraka.FredKlabu ya Manchester United wanatajwa kujiandaa na kuondoka kwa kiungo Fred ambapo inaelezwa atakapoondoka kiungo huyo wa Brazil tu itakua ndio nafasi na wakati sahihi wa kutuma ofa kwa klabu ya Fiorentina kwajili ya kiungo Sofyan Amrabat.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa