Mane Kuelekea Al Nassr ni Suala la Muda

Mshambuliaji wa klabu ya Bayern Munich na timu ya taifa ya Senegal Sadio Mane aanatajwa kumalizana na klabu ya Al Nassr kutoka nchini Saudia Arabia.

Mane anatajwa kumalizana na klabu ya Al Nassr siku kadhaa zilizopita kwenye maslahi binafsi na kilichokua kinasubiriwa zaidi ni ofa ya Al Nassr kwa Bayern Munich ambapo mpaka sasa inaelezwa vilabu hivo vimeshakubaliana.ManeWinga huyo wa zamani wa Liverpool amekua hana msimu mzuri ndani ya kikosi cha Bayern Munich kutokana na majeraha ambayo yamekua yakimuandama na ndio sababu mabingwa hao wa Ujerumani wameamua kuachana nae.

Mshambuliaji Sadio Mane alikua moja ya wachezaji wanaolipwa mishahara mikubwa zaidi ndani ya klabu ya Bayern lakini ubora wake haukua mkubwa ndani ya timu hiyo lakini klabu ya Al Nassr wamemuahidi mshahara mkubwa zaidi.ManeSababu nyingine iliyopelekea staa huyo kutimka ndani ya klabu ya Bayern Munich ni kutokua kwenye mipango ya kocha wasasa wa klabu hiyo Thomas Tuchel ambaye alijiunga na klabu hiyo mapema mwaka huu.

Acha ujumbe