Mane Asimamishwa Bayern

Mchezaji wa klabu ya Bayern Munich raia wa kimataifa wa Senegal Sadio Mane amesimamishwa kuendelea kuitumikia klabu hiyo baada ya tukio lake la kumshambulia mchezaji mwenzake ndani ya timu hiyo Leroy Sane.

Mshambuliaji Sadio Mane ameripotiwa kumpiga ngumi usoni mshambuliaji mwenzake wa klabu hiyo Leroy Sane kwenye vyumba vya kubadilishia nguo baada ya kua na majibazano uwanjani katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya klabu ya Manchester City siku ya jumanne usiku.maneBaada ya kitendo alichokifanya mshambuliuaji huyo klabu ya Bayern Munich imetoa taarifa kua mchezaji huyo atafungiwa kwa muda kutocheza mchezo wowote wa klabu hiyo ikiwemo mchezo wa wikiendi hii dhidi ya Hoffeinhem kwenye ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga.

Sadio Mane pia inaelezwa atapigwa faini kutokana na kitendo ambacho kimetokea cha kumshambuliaji mchezaji mwenzake, Huku mpaka sasa chanzo rasmi cha ugomvi kati ya nyota huyo wa zamani wa Liverpool dhidi ya Leroy Sane kikiwa hakijajulikana au kuwekwa wazi.maneMshmbuliaji Sadio Mane amekua hana wakati mzuri ndani ya klabu ya Bayern Munich siku za karibuni baada ya kutoka kwenye majeraha, Vyanzo mbalimbali kutoka nchini Ujerumani vimeanza kuripoti mchezaji huyo hana furaha klabuni hapo wengne wakimuhusisha kurudi ndani ya Liverpool.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.