Dembele Kutimkia PSG

Mchezaji wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Ufaransa Ousmane Dembele anatajwa kutimkia klabu ya PSG mabingwa wa ligi kuu ya soka nchini Ufaransa.

Ousmane Dembele amekua akitajwa kujiunga na klabu ya PSG tangu mzimu uliomalizika, Lakini msimu huu mabingwa hao wa Ufaransa wanaelezwa kupiga hatua kunasa saini ya winga huyo wa klabu ya Barcelona.dembeleKlabu ya PSG chini ya kocha Luis Enrique inataka kutengeneza timu bora ya muda mrefu, Ambapo kocha huyo anajitahidi kusajili wachezaji wenye uwezo mkubwa lakini ambao umri wao sio mkubwa sana kwajili ya mipango ya muda mrefu.

Klabu ya Barcelona wao wanapitia kipindi kigumu kiuchumi na wanaelezwa kumpa Dembele ofa ya mkataba mpya, Lakini uhakika mkubwa ni kua ofa ya Barcelona sio kubwa kama ya PSG hivo kuna uwezekano mkubwa mabingwa hao wa Ufaransa wakamshawishi mchezaji huyo.dembeleFaida nyingine ambayo wanaipata PSG ni kuhakikisha wanapata saini ya mchezaji huyo mapema ambapo mpaka hela ya kumnunua ni euro milioni 50 mpaka mwezi huu tarehe 31 lakini kuanzia baada ya hapo inapanda mpaka euro milioni 100.

 

Acha ujumbe