Bondia wa uzani wa Super Welter kutoka Tanzania, Hassan Mwakinyo amepanda katika viwango vya ubora wa dunia na kuingia katika nafasi kumi bora za uzani huo.

Mwakinyo alikuwa katika nafasi ya 11 baada ya pambano lake la mwisho lililochezeka hapa Tanzania, na sasa amepanda nafasi moja mpaka nafasi ya 10 kati ya mabondia 1,530 wa uzito huo duniani.
Katika ukurasa wake wa Twitter, Mwakinyo ameandika “Alihamdulilah Rank Imesoma Tena.
“Tumeingia 10 bora kwenye viwango vya ubora Duniani kwa mabondia wa uzani wa Super Welter , kutoka nafasi ya 11 sasa nashika nafasi ya 10 kati ya mabondia 1,530 wa uzani huo.” aliongeza mwanamasumbwi huyo.

Fanya wiki yako iwe ya kuvutia zaidi, tunaelekea Los Angeles kutengeneza mkwanja na kasino maridhawa ya LA Rouge kutoka katika kasino za mtandaoni za meridianbettz, Fursa ya kufurahi huku unajaza pochi yako.

CHEZA HAPA

