Mzee Ally Pazi Samatta amesema kama Simba ingeishinda Yanga wikiendi iliyopita, wangemtambua Bernard Morrison.
Ally ambaye ni Baba wa straika namba moja wa Tanzania, Mbwana Samatta amesema akili ya kazi ya Morrison imekomaa licha ya kwamba ni mchezaji aliyeongoza kwa kuzomewa lakini hakujali zaidi ya kutimiza majukumu aliyopangiwa na kocha wake Didier Gomes.
“Ndani ya kikosi mkiwa na wachezaji saba kama Morrison timu hiyo inakuwa tishio, anajua yeye ni nani katika majukumu yake, ndicho alichokifanya kwenye mchezo wa watani, Yanga ndio ilikuwa na presha kipindi cha pili kutokana na Simba kufika langoni kwao mara kwa mara, huku Morrison akitumia akili kubwa kutengeneza faulo nyingi,”
Amesema bahati mbaya Simba, ilipoteza mechi lakini ingeshinda anaamini Morrison angekuwa habari ya mjini kwa kuzungumziwa zaidi alichokifanya.
“Kama unavyojua mechi za Simba na Yanga zinavyoongoza kwa mihemko na ndio maana hatajwi Mauya aliyewapa raha wanamtaja mzee Mpili, ila kiuwezo Simba ingeshinda na angefunga Morrison angekuwa habari ya mjini,” alisema.
IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!

