Nagelsmann Mbioni Kua Kocha Mkuu Ujerumani

Shirikisho la soka nchini Ujerumani maarufu kama DFB liko mbioni kumalizana na kocha wa zamani wa vilabu vya Bayern Munich na Rb Leipzig Julian Nagelsmann kuifundisha timu ya taifa ya Ujerumani.

Kocha Nagelsmann alikua kwenye orodha ya juu kabisa ya makocha ambao wanahitajika kuifundisha timu ya taifa ya Ujerumani ambayo ilikua chini ya kocha wa zamani wa Bayern Munich Hans Flick.nagelsmannTimu ya taifa ya Ujerumani haipo kwenye kiwango bora kwenye miaka ya hivi karibuni wakiwa hawajafanya vizuri kwenye michuano mikubwa mitatu iliyopita mpaka sasa chini ya makocha wawili ambao wamefukuzwa kwasasa.

Kocha Hans Flick aliendelea alipoishia mwenzake Joachim Low ambaye alitolewa kwenye michuano ya kombe la dunia 2018 hatua ya makundi na Euro 2020 hatua ya robo fainali,Huku Flick nae akitolewa hatua ya makundi kombe la dunia 2022 na mwenendo mbaya ambao umemfanya akafukuzwa.nagelsmannKocha Julian Nagelsmann ambaye aliondolewa na Bayern Munich mwezi Machi mwaka huu ameonekana na DFB kama mtu sahihi wa kukinoa kikosi hicho cha Ujerumani maarufu kama Bavarians kuelekea michuano ya mataifa ulaya mwakani inayotarajiwa kufanyika kwenye ardhi yao.

 

Acha ujumbe