Klabu ya Newcastle United leo itashuka dimbani katika uwanja wake wa St.James Park ambapo wataikaribisha klabu ya Tottenham katika mchezo wa kuwania nafasi nne za juu katika ligi kuu ya Uingereza.
Newcastle mpaka sasa wanashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza huku Tottenham wakikamata nafasi ya tano, Hivo mchezo huo unaenda kua wenye mvuto kutokana na kila timu kuhitaji kushinda mchezo huo ili kuendelea kujiwekea mazingira mazuri ya kufuzu ligi ya mabingwa barani ulaya msimu ujao.
Vilabu hivyo mpaka sasa vimeachana kwa jumla ya alama tatu mpaka sasa kwani vijana wa kocha Eddie Howe wana alama 56, Huku Tottenham wao wakiwa na alama 53 hivo ni alama tatu tu mpaka sasa ambazo zimewatenganisha ambazo zimempa mmoja fursa ya kukaa juu ya mwenzake.
Klabu ya Newcastle ambayo imetoka kupoteza mchezo wikiendi iliyopita dhidi ya Aston Villa katika dimba la Villa Park na kuwafanya kushuka hadi nafasi ya nne kwenye msimamo leo watahitaji alama tatu wakiwa nyumbani ili kurejea kwenye nafasi tatu na kukaa juu ya Manchester United.
Tottenham wanaingia kwenye mchezo wa leo pia wakiwa na kumbukumbu za kupoteza dhidi ya Bournamouth wikiendi iliyomalizika, Lakini watauhitaji mchezo huu kuhakikisha wanalingana alama na Newcastle United ambao wapo juu yao kwa alama tatu, Kwani lengo kubwa kwasasa kwa klabu hiyo ni kufuzu ligi ya mabingwa barani ulaya msimu ujao.

