Nusu Fainali Ya French Open Kutimua Vumbi Leo.

 

Nusu Fainali ya michuano ya French Open inatarajiwa kutimua vumbi leo katika viwanja vya Stade Roland Garros kule Paris, Ufaransa.

Nusu fainali ya kwanza ya French Open inawakutanisha Rafael Nadal na Alexander Zverev na ile ya pili iwakutanisha Casper Ruud na Marin Cilic.

 

Katika robo fainali ya michuano hiyo, siku ya Jumanne Nadal alimtoa bingwa wa Italian Open, Novak Djokovic wakati Zverev akimtoa Alcaraz Garfia na kutinga nusu fainali.

Robo fainali nyingine iliwakutanisha Ruud ambaye alimtoa Rune na Cilic akimtoa Rublev na kujihakikishia nafasi ya kutinga nusu fainali siku ya Jumatano.

Fainali ya French Open itapigwa siku ya Jumapili majira ya saa kumi jioni katika viwanja vya Stade Roland Garros kule Paris, Ufaransa.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

Acha ujumbe