Ole Gunnar Solskjaer: Kane Alikua Tayari Kuja United

Kocha wa zamani wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amesema kua mshambuliaji wa klabu ya Bayern Munich na timu ya taifa ya Uingereza Harry Kane alikua tayari kujiunga na Man United.

Ole Gunnar Solskjaer amesema alikua anamuhitaji mshambuliaji huyo wa zamani wa Tottenham Hotspurs na aliieleza bodi ya Manchester United juu ya kumsajili mchezaji huyo lakini timu haikua na bajeti ya kutosha.ole gunnar solskjaerKocha huyo anasema jambo lililokwamisha klabu ya Manchester United kushindwa kumsajili Harry Kane ni tatizo la kifedha ambalo klabu hiyo ilikua inapitia haswa kipindi cha mlipuko wa ugonjwa wa Covid 2019.

Mshambuliaji Harry Kane inaelezwa hata dirisha kubwa lililopita alikua ndio chaguo la kwanza la kocha Erik Ten Hag, Lakini alikua anaigharimu klabu hiyo kiwango kikubwa cha pesa na ndio sababu ya kujitoa kwenye mbio za kumuhitaji mshambuliaji huyo.ole gunnar solskjaerSiku ya jana Harry Kane alieleza kua dirisha kubwa lililopita klabu moja tu ndio alitaka kujiunga nayo, Lakini Ole Gunnar Solskjaer amesema mshambuliaji huyo alikua yupo tayari kujiunga na klabu hiyo muda mrefu uliopita lakini ukosefu wa hela ndio ulikwamisha dili.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.