Olise Asaini Mkataba mpya Palace

Winga wa klabu ya Crystal Palace Michael Olise amefanikiwa kusaini mkataba mpya na klabu yake hiyo ambapo utamuweka klabuni hapo kwa miaka minne zaidi mbele.

Winga huyo raia wa kimataifa wa Ufaransa alikua anafukuziwa na klabu ya Chelsea na ikielezwa wanakaribia kumpata mchezaji huyo,Lakini taarifa za kutoka klabu ya Crystal Palace ni kua mchezaji huyo ameongeza mkataba mpya.oliseMichael Olise amekubali kusaini kandarasi mpya na klabu ya Palace baada ya mazungumzo ya muda mrefu na klabu hiyo, Hivo hii inaonesha vilabu vyote ambavyo vilikua vinafukuzia saini ya winga huyo vitahitajika kuvunja mkataba ili kupata saini yake.

Klabu ya Chelsea wamekua wakifanya usajili wakutisha siku za hivi karibuni ambapo baada ya kukamilisha usajili wa Moises Caicedo na Romeo Lavia na kituo kinachofuata kilikua kwa winga huyo raia wa kimataifa wa Ufaransa.oliseMchezaji Michael Olise amekua kwenye kiwango kikubwa ndani ya klabu ya Crystal Palace, Hivo kupelekea klabu hiyo kumuongezea mkataba mpya ambao utamuweka zaidi klabuni hapo licha ya kufukuziwa na vilabu kadhaa.

 

Acha ujumbe