Pape Sakho 🇨🇲 amezaliwa 21 December 1996, nchini Senegal akiwa na miaka (24). Mchezaji mwenye kiwango kikubwa na uwezo akicheza nafasi ya winga wa kushoto.

Pape Sakho alianza maisha yake ya kucheza soka mwaka 2017, kwenye klabu ya Diambars Fc ya Senegal akicheza nusu msimu, Pape msimu wa 2017/2018 alijiunga na klabu ya Mbour P.C kwa uhamisho huru akidumu mwaka mmoja.
Mnamo majira ya kiangazi mwaka 2019, Pape alijiunga na moja ya timu ya daraja la pili nchini Ufaransa na kudumu mwaka mmoja, winga huyu Pape Ousmane Sakho alirejea tena kwenye ligi ya nyumbani na kujiunga na timu ya Teungueth FC na kudumu kwa mwaka mmoja.
Wasenegali kule kwao wanamfananisha na mchezaji wa klabu ya Liverpool, Sadio Mane. Wasenagali wengi hawakutarajia kama Sakho angejiunga na Simba SC matarajio yao yalikuwa kumuona Pape Sakho akitimkia Ulaya.
Pape Sakho alionesha kiwango kikubwa sana msimu wa 2020/2021. Mpaka sasa skiwa na Simba SC amecheza mechi nne amefunga mabao matatu na assist moja.
Unaanzaje siku yako na kuimaliza bila kupitia katika kasino bomba za meridianbettz, mchezo mashuhuri wa Disco Funk unaweza kukufanya uwe mshindi leo hii.!


