Mchezaji wa kimataifa wa Argentina Roberto Pereyra amesaini rasmi mkataba mpya wa Udinese, akirejea klabuni hapo baada ya mkataba wake wa awali kumalizika mwezi Juni.

Kiungo huyo mbunifu amekuwa mchezaji huru tangu kandarasi yake ilipomalizika Juni 30 na alihusishwa na timu nyingine kadhaa, zikiwemo Cagliari, Salernitana, Parma, Palmeiras na pande za Saudi Arabia.
Aviator, poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Piggy Party na mingine kibao upige pesa na Meridianbet. Ingia www. meridianbet.co.tz.
Hata hivyo, leo amerejea Dacia Arena na kusaini mkataba mpya wa mwaka mmoja kwa Udinese.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 alikuja Italia kwa mara ya kwanza kwa Udinese mnamo 2011, alibaki hadi kuhamia Juventus mnamo 2014, kisha akarejea kutoka Watford mnamo 2020.
Tucu Pereyra aliichezea Friulani mechi 200 za ushindani, na kuzifumania nyavu mara 23 akiwa na asisti 33.
Ukiwa na meridianbet odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti.

Akiwa mchezaji huru, bado aliweza kusajiliwa na Udinese hata baada ya dirisha la uhamisho kukamilika.

