Raisi wa Real Madrid, Florentino Perez amezungumzia sakata la kocha aliyeondoka Zinedine Zidane na beki kisiki Sergio Ramos baada ya kimya kirefu.
“Ramos ni kama Mtoto wangu namjua vyema na nilimleta mimi hapa, iliniuma pia siku anaondoka Madrid kama Baba” alisema Perez
“Kijana wangu hakutaka tu kusema ukweli, tulimpa mkataba na ulikuwa na deadline ila yeye hakuzingatia. Siku moja Ramos atarejea Bernabeu, atarejea kwa nafasi nyingine hilo nina uhakika nalo.
“Kuhusu Zidane nilifahamu kuwa ataondoka, namfahamu vizuri sana ni Kijana wangu, nilimbembeleza abaki ila hakutaka. Zidane ana ndoto za kuwa Kocha wa timu ya Taifa ya Ufaransa, nazifahamu hizo ndoto zake.
“Real Madrid ni nyumbani kwake, kama siku Zizzou anataka kurejea basi milango ipo wazi siku zote. Kuhusu barua yake wakati anaondoka wala sikuisoma, najua hakuandika yeye na ule sio mwandiko wake, kuna mtu alimwandiki.” aliongeza Perez katika Press aliyoifanya na vyombo vya habari.
Hakuna mipaka ya ushindi kwenye Keno Instant ya meridianbet Kasino, hii wewe ndiyo una uamuzi zaidi juu ya mchezo na nafasi ya machaguo kibao.


