Aliyekuwa kocha wa Yanga SC, Mholanzi Hans Van Der Pluijm amethibitisha kuwa amejipanga kuwafungulia mashitaka klabu hiyo kwa Shirikisho la Soka Duniani FIFA kuhusiana na madai ya stahiki zake.
Pluijm amesema: “Taarifa za za mimi kuwa kwenye mpango wa kuwapeleka Yanga FlFA ni za kweli, lakini nisingependa kuzungumza sana kuhusu suala la kesi hii kwa sasa, kwakuwa kuna wawakilishi wangu ambao wako Dar es Salaam kwa sasa wanashughulikia kesi hii.”
Inaripotiwa kuwa kocha huyo anaidai Yanga SC kiasi kinachokadiriwa kuwa dola 50,000 (TSh milioni 115) ambazo amekuwa akitumikia kikosi hicho kwa kipindi chote klabuni hapo.
Unaanzaje siku yako bila kuwa na pesa, Meridianbet kupitia kasino zake za mtandaoni inakupa sababu ya kufanya siku yako kuwa njema. Mchezo maarufu wa Tiki Reward unaweza kukufanya milionea. Cheza sasa kibingwa!


