Tangu kuanza kwa mwaka 2022, kwa baadhi ya wachezaji na vilabu, hii ni fursa ya kufanya biashara huru. Mauricio Pochettino anaimani na nyota wake, Kylian Mbappe.
Mbappe ni miongoni mwa wachezaji nyota ambao wamebakiza miezi 6 tu mikataba yao kumalizika kwenye vilabu walivyopo kwa sasa. Katika mazingira haya, mchezaji anaruhusiwa kuzungumza na kusaini mkataba na klabu yeyote nje ya ligi anayocheza kwa sasa.
Mbappe, Cavani, Pogba, Rudiger na Insigne ni miongoni mwa wachezaji nyota ambao mikataba yao imefikia kwenye hatua hii. Kwa Mbappe, kocha wa PSG, Mauricio Pochettino anaimani nae.

Poch amenukuliwa akisema;
Klabu [PSG] inajua hali yake [Mbappe]. Ni matamanio yetu kuwa atabaki hapa na kuendelea kuwepo kwa miaka kadhaa ijayo.
Tunategemea kumuona Kylian akiendelea kuonesha ubora wake na hivyo, ni matokeo yake ni mazuri kwa kila mmoja.
Endapo suala la mkataba mpya litashindwa kufikiwa muafaka kati ya Mbappe na PSG, mchezaji huyo ataondoka huru mwishoni mwa msimu huu. Real Madrid wanatajwa kama timu inayomuwinda nyota huyu kwa muda mrefu.
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.


