Pochettino Kuwafikirisha Man United

Kuelekea mwishoni mwa msimu huu, Mauricio Pochettino anaendelea kuichachafya Manchester United katika mchakato wa kumsaka kocha mpya.

Pochettino amekuwa akihusishwa na United toka 2016, wakati ule alikuwa kocha wa Tottenham Hotspur. Japokuwa hakuwahi kupatiwa nafasi hiyo kule Old Trafford, kuna uwezekano mwaka huu ukawa ni wake.

United inahaha kumpata kocha mpya wa muda mrefu ambaye ataiongoza klabu hiyo kuanzia majira ya joto mwaka huu. Wakati mchakato wa kumtafuta kocha ukiwa umeanza kama alivyoripoti Mkurugenzi wa Michezo, John Murtough, inasemakana Mauricio anaanza kuonesha utata wake.

Inasemakana, Mauricio ataifikiria kazi ya United endapo tu, klabu hiyo itamshawishi kuwa yeye ndio chaguo lao la kwanza. Hii ikiwa inamaana kuwa, kocha huyu hatoifikiria kabisa United kama watakuwa wanamchukulia kama mbadala wa kocha mwingine yeyote wanayempa nafasi ya kwanza kwenye mchakato wao.

Naam, waswahili wanasema “ijue thamani yako na uilinde”. Hiki ndicho anachokifanya Poch ambaye anajumuishwa na Erik Ten Hag kwenye orodha ya makocha wanaopewa nafasi ya kuiongoza Man United kuanzia majira ya joto mwaka huu.


VUNA MKWANJA NA SHINDANO LA EVOPLAY SPRING AWEKING

Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000  katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

Acha ujumbe