Pochettino:Palmer Kuongezewa Kandarasi

Kocha wa klabu ya Chelsea Mauricio Pochettino amesema kua kiungo mshambuliaji anayekipiga klabu hiyo akitokea Manchester City Cole Palmer anastahili kuongezewa mkataba.

Wakati akihojiwa na wanahabari kuhusu Cole Palmer kupewa kandarasi mpya alisema”Anafanya vizuri lakini amesaini mkataba wa miaka mitano, sita, saba sijui” Lakini kama timu itaona kuna haja ya kufanya hivo itafanya hivo”pochettinoKiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza amesaini mkataba wa miaka saba ndani ya klabu ya Chelsea na kipengele cha kuongeza mkataba wa mwaka mmoja, Lakini kocha huyo ameweka wazi kua kama timu itaona kuna uwezekano wa kumuongezea tena mkataba itafanya hivo.

Akiwa ana miezi takribani nane ndani ya klabu ya Chelsea Cole Palmer amefanya kazi kubwa sana ndani ya klabu hiyo, Huku mpaka sasa akioneakna kama mchezaji bora ndani ya klabu hiyo, Lakini pia akitabiriwa kuchukua tuzo ya mchezaji bora kijana wa ligi kuu ya Uingereza.pochettinoKiungo Palmer ni wazi amekua na msimu bora sana ndani ya klabu hiyo jambo ambalo limewafanya hata mashabiki wa klabu hiyo kutamani aongezewe mkataba mwingine licha ya kusiani miaka saba, Jambo ambalo kocha Pochettino amesema linawezekana kama klabu itaona ni jambo sahihi.

Acha ujumbe