Kocha wa klabu ya Chelsea Mauricio Pochettino ameweka wazi kua mshambuliaji wa klabu hiyo Christopher Nkunku hatokuepo kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Man United.
Christopher Nkunku ambaye ameshaanza mazoezi mepesi na klabu hiyo baada ya kua kwenye majeraha ya muda mrefu, Lakini kocha Pochettino ameeleza mchezaji huyo hatakua tayari kwa mchezo wa kesho.Mashabiki wengi wa klabu ya Chelsea walitarajia huenda mshambuliaji hjuyo angekuepo kwenye sehemu ya kikosi kitakachosafiri kwenda kuikabili Man United, Lakini haijawa kama walivyotarajia kwani kocha ameeleza mchezaji huyo bado hajakua tayari kucheza.
Kitu kinachoonekana kwa klabu ya Chelsea ni kua hawataki kuharakisha kumchezesha mchezaji huyo, Kwani wanahitaji Nkunku apone majeraha yake kwa asilimia 100 kwani kumharakisha kurejea uwanjani kunaweza kumsababishia kupata majeraha tena.Kocha Mauricio Pochettino amesisitiza mshambuliaji Christopher Nkunku atarejea kiwanjani hivi karibuni, Lakini sio kwa mchezo wa kesho mshambuliaji huyo amekua akifanya mazoezi kwa takribani wiki mbili sasa ni wazi atarejea katika kikosi hivi karibuni.