Varane, Johnny Evans Warejea Mazoezini

Kocha wa Manchester United ameeleza kua mabeki wake wawili waliokua wanauguza majeraha ambao ni Raphael Varane na Johnny Evans wamerejea mazoezini leo.

Mabeki Raphael Varane na Evans walikua wanasumbuliwa na majeraha katika michezo iliyopita, Lakini kocha Ten Hag ameweka wazi kua wachezaji hao wamerejea mazoezini mapema leo jambo ambalo limepokewa vizuri na benchi la ufundi la klabu hiyo.varaneKurejea kwa mabeki hao kunaongeza nguvu kwenye kikosi hicho baada ya taarifa ya majeraha ndani ya kikosi hicho kutoka jana, Ambapo mabeki Lisandro Martinez pamoja na Victor Lindelof watakosekana uwanjani kwa muda wa mwezi mmoja.

Beki Harry Maguire ambaye na yeye alikua akiandamwa na majeraha baada ya kwenda kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Uingereza amerejea mazoezini jana, Hivo licha ya kukosekana kwa Lisandro Martinez na Lindelof lakini kuna mabeki watatu wa kati watakua sawa kuitumikia timu hiyo.varaneMabeki Raphael Varane, Johnny Evans, pamoja na Harry Maguire watakua watu muhimu sana kuelekea mchezo wa kesho wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Chelsea utakaopigwa kesho, Ambapo mabeki hao wanaweza kuunda safu ya ulinzi ya timu hiyo.

Acha ujumbe