Klabu ya soka ya Ufaransa, Paris Saint-Germain (PSG) wametozwa faini ya Sh3.7 milioni kwa hatia ya kutorejea uwanjani kwa wakati uliostahili baada ya mapumziko ya kipindi cha kwanza walipokuwa wakivaana na Atalanta kwenye robofainali ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA).
PSG waliibuka washindi wa mechi hiyo iliyochezewa jijini Lisbon, Ureno mnamo Agosti 12, 2020 na hivyo kujikatia tiketi ya kuvaana na RB Leipzig ya Ujerumani kwenye hatua ya nusu-fainali kwa mara ya kwanza baada ya miaka 25. Nusu-fainali hiyo itapigiwa jijini Lisbon mnamo Agosti 18, 2020.
Leipzig waliwabandua Atletico Madrid ya Uhispania kwenye hatua ya nane-bora kwa mabao 2-1, hii ikiwa idadi sawa ya mabao ambayo PSG walifunga dhidi ya Atalanta ya Italia.
Kocha Thomas Tuchel wa PSG pia ameonywa vikali na Uefa kwa kutowajibika ipasavyo na kuchangia kukawia kuanzishwa kwa kipindi cha pili wakati wa mechi dhidi Atalanta. Mechi hiyo ilicheleweshwa kwa dakika saba.
Uefa inawaadhibu PSG siku moja baada ya kuwatoza Sevilla faini ya Sh1.2 milioni kwa kuchelewa kufika uwanjani wakati wa mechi ya robo fainali ya Europa League iliyowakutanisha na Wolves mnamo Agosti 11, 2020.
Sevilla ambao ni mabingwa mara tano wa kipute cha Europa League, waliwapokeza Wolves kichapo cha 1-0 katika mechi hiyo iliyowakatia tiketi ya kupepetana na Manchester United kwenye nusu fainali itakayoandaliwa mjini Dusseldorf, Ujerumani mnamo Agosti 16, 2020.
Umekuwa mteja muaminifu wa meridianbet? Basi fahamu kuwa kuna zawadi kibao hadi 5% ya pesa yako inarejeshwa kwako. Kila wiki unaweza kurudishiwa mpaka Tsh 250,000.
Rose kapinga
Sheria ni msumeno lazima ifuatwe!!!
Ester jackson
Nimependa sana sheria za michezo kwa wezetu wako vizuri kama ingekuwa kwetu kwa kweli ingekuwa iko vizuri sana na wawekezaji wangeongezeka zaidi ila hili hamna
Zeiyana
Makosa yapo ila kuna mkosa mengine yaangaliwe bac jamani. ukiangalia na ali ya uchumi sas hivi imepolomoka sana
Sauda
Ni sawa, ili iwe fundisho kwa wengine
Caroline
Itakua fundisho kwao na kwa wengine
Tatu
Sheria ifuatwe mkondo wake
rama
Maoni:sawa kabisa katika jili wenzetu ulaya hawajali ukubwa wa timu wanaitaji nidhamu
felister
vizuri hii iwe fundisho kwao na kwa vilabu vyengine
Lydia Emmanuel Magoti
PSG inatakiwa wawe makini zaidi
Mwajumah
Vizuri ili iwe fundisho kwao na kwa vilabu vingine#Meridianbettz
Ernest
Naona UEFA Wamepata njia ya kuvuna mkwanja baada ya Corona kutikisa ulimwengu sasahivi ukizingua kidogo unapitiwa na Rungu la UEFA
Sadick
Taasisi yoyote lazima iwe na utaratibu unaotakiwa kufuatwa na kuheshimiwa na watu wote. Hongera UEFA kwa kuendelea kupiga rungu timu zote zinazokiuka utaratibu#meridianbettz
Sabrina
Pole Sana PSG Ila wanatakiwa kujifunza kutokana na makosa
aisha
Poleni sana psg lakini ndivyo ilivyo lazima tujifunze kutokana na makosa pia haitojirudia tena
Njiku
Safii sana hii itakuwa kama funzo kwa timu zingine ambaozo zitakazo Keuka sheria na taratibu zote ambazo zilizowekwa kwa kufuatwa na kila timu kwangu hii imekaa poa sanaa watoto mabishoo wengi sijui wanaenda na vioo na vitana
Ester mmakasa
Psg wamewaangusha mashabiki wao sana.
Nasra
Sheria zilizowekwa lazima zizingatiwe na vilabu vyote ulimwenguni.
Dorophina
Hilo ni funzo kwa wengine makosa yasijirudie
Saupha mohamed
Hii fundisho kwa wengine
Fatina mfingi
Hi ni sawa ili club nyingine zipatae fundisho
Mwanahamisi
Sheria ifuate mkondo wake ili iwe fundisho kwa wengine
Samiah
Nifundisho kwa wengine
Shafii
Litakua fundisho kwa vilabu vyote kuto heshimu sheria na kanuni zilizowekwa.
julie
safi sana
Issa
Wapate adhabu iwe fundisho pia kwa wengine
Janeflora malisa
Ni moja ya fundisho
Furahav
Duuh noma Sana.
Devotha
UEFA wamepamba moto timu ikitereza kidogo tu fain
Hope mwaikuka
Ni vzur wajfunze siku nyngne
Povel
Duh Haki itendeke hapo
David Pere
Nimependa sana sheria za michezo kwa wezetu wako vizuri kama ingekuwa kwetu kwa kweli ingekuwa iko vizuri sana na wawekezaji wangeongezeka zaidi ila hili hamna
Latifa juma mohamed
Sawa sheria ifuatwe watajifunza kwa Hilo.
farida ahmadi
Lazima hatua za kisheria za mpira zifatwe
warda
Jamani Pesa yote hii!!!Imeniuma kama nimetoa mie#Meridianbettz
magdalena
fundisho kwa wengine ata hao psg siku nyingine watatii muda
Neema
Sheria ifuate mkondo wake
Shan
Ni mfano mzuri kwa timu zisizo zingatia sheria.
Gabriel
Duuh! Wenzetu wanasheria kal sana maana ata sevilla walipewa faini walipochelewa kureport uwanjan bac n Jambo la kuigwa hata TFF wanatakiwa wajifunze kupitia wenzetu
Khadija
sheria ni msumeno lazima ifatwe
Salma ngende
Sheria razima izingatiwe
Genia Sikaluzwe
Lazima Sheria zifatwe
Christa
Mpira una sheria, wanatakiwa kuzifuata
Theonestina
Duuuh atar Sana