Rashford: Hatujakata Tamaa

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester Marcus Rashford amesema kua hawajakata tamaa baada ya kupoteza mchezo wa ligi kuu ya Uingereza wikiendi iliyomalizika dhidi ya mahasimu wao klabu ya Liverpool.

Marcus Rashford ameweka kua ni ukweli walikua chini ya kiwango kama timu siku ya jumapili na kupelekea kupokea kichapo kizito dhidi ya klabu ya Liverpool siku ya jumapili, Lakini amesema sio sababu ya kukata tamaa kuelekea michezo mingine inayofuta mbele yao.RashfordRashford anasema kua ameumizwa na kipigo walichokipata na baada ya mchezo aliandika kwenye mitandao yake ya kijamii siku inayofuata kua anatamani wangecheza tena ili waweze kuweka vitu sawa, Lakini mshambuliaji huyo alimuambia muandishi hawana cha kufanya tena kwasasa zaidi ya kuangalia mbele na kuachana na yaliyopita.

Klabu ya Manchester United baada ya kua kwenye fomu ya hali ya juu lakini walijikuta wakiangukia pua dhidi ya klabu ya Liverpool ambayo ilionekana kutokua kwenye kiwango bora sana kwasasa, Lakini iliweza kupata matokeo makubwa dhidi ya mashetani wekundu hao katika dimba la Anfield.RashfordMshambuliaji Marcus Rashford anaamini kua wachezaji wenzake watarudi kwa nguvu katika michezo mingine ambayo inafuata, Kwani mipango yao msimu huu ni kushinda mataji na tayari wameshafanikiw akushinda taji moja hivo akili yao ipo kwenye michezo inayofuata mbele.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.