Klabu ya Manchester United ipo tayari kusikiliza ofa kutoka kwa vilabu pinzani vya Ligi Kuu England kwa ajili ya Marcus Rashford, iwapo Barcelona watashindwa kukamilisha dili la kumsajili moja kwa moja. Mshambuliaji huyo kwa sasa yupo kwa mkopo Camp Nou, lakini hali ya kifedha ya Barcelona imeweka sintofahamu juu ya mustakabali wake.

Kwa mujibu wa makubaliano ya mkopo, Barcelona wana chaguo la kumnunua Rashford kwa euro milioni 30. Hata hivyo, United wameweka wazi kuwa hawatakuwa tayari kupunguza dau hilo wala kukubali masharti mapya kama kuchelewesha malipo au kuongeza muda wa mkopo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Rashford ameonyesha kiwango kizuri nchini Hispania, akifunga mabao 10 katika mechi 39, jambo lililoongeza thamani yake sokoni. Hali hii imeifanya Manchester United kuwa na nguvu zaidi ya kujadiliana, wakiamini wanaweza kupata ofa kubwa zaidi kutoka kwa vilabu vingine, hasa ndani ya England.
Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona, Deco, amekiri kuwa uamuzi wa kumbakiza Rashford unategemea mambo kadhaa ikiwemo sheria za matumizi ya fedha, mahitaji ya timu na maamuzi ya benchi la ufundi. Naye rais wa klabu, Joan Laporta, amedokeza uwezekano wa kuongeza muda wa mkopo badala ya kununua moja kwa moja.

Iwapo Barcelona watashindwa kufanikisha uhamisho huo, Manchester United wanaamini watapata ofa kutoka kwa vilabu vya England, jambo litakalowawezesha kupata faida kubwa zaidi. Hata hivyo, bado kuna uwezekano mdogo wa Rashford kurejea Old Trafford, hasa baada ya mabadiliko ya benchi la ufundi chini ya Michael Carrick.

