Beki wa kulia wa klabu ya Chelsea Reece James raia wa kimataifa wa Uingereza huenda akaukosa msimu uliobakia ndani ya klabu hiyo kutokana na majeraha ya misuli ya paja aliyoipata.
Beki Reece James amekua akisumbuliwa na majeraha tangu msimu huu uanze na kumfanya mpaka kukosa michuano ya kombe la dunia iliyopigwa nchini Qatar mwaka jana, Lakini beki huyo alirejea na kuendelea kuitumikia klabu yake kwenye michezo kadhaa kabla ya kupata majeraha tena.
Kocha Frank Lampard wakati akizungumza na waandishi wa habari leo mapema kuelekea mchezo wao wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Brentford amesema beki huenda akakosekana kwa msimu uliobakia kutokana na majeraha ya misuli ya paja ambayo ameyapata.
Beki Reece James amekua moja ya wachezaji muhimu ndani ya klabu ya Chelsea kwa misimu mitatu sasa, Lakini msimu huu imekua tofauti kidogo kwani mchezaji huyo amekua akiandamwa na majeraha mara kwa mara na kufanya kukosekana katika michezo mingi ya timu hiyo.
Kutokana na kauli ya kocha Frank Lampard juu ya beki Reece James ni wazi kuna uwezekano mkubwa beki huyo kukosekana ndani ya klabu hiyo kwa msimu wote uliobakia, Hii inaendeleza rekodi yake mbaya ya majeraha ambayo amekua nayo kwa msimu huu ndani ya klabu hiyo.

