Mchezaji wa Borrusia Dortmund Marco Reus ana uhakika kuwa wameacha historia mbaya msimu uliopita kwenye ligi ya mabingwa ambapo walitolewa kwenye kundi mapema licha ya kuwa na mshambuliaji mahiri barani Ulaya Erling Haaland.

Reus anasema walianza vizuri kwa ushindi dhidi ya Besktas ya Uturuki na Sporting Lisbon FC na baadae kupoteza michezo mitatu mfululizo ikiwemo kupokea kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa Ajax inayoshiriki ligi kuu ya Netherlands.
Dortmund ataanza kampeni ya ligi ya mabingwa msimu huu kwa mechi ya nyumbani dhidi ya Copenhagen ambayo itakuwa ni mechi ya ushindani kati ya hizo timu mbili.
Katika mechi tano za Bundesliga Dortmund wameshinda mechi nne na kupoteza moja huku wakiwa na fomu nzuri. Reus amesema hakuna kitu kitakachowakatisha tamaa kutoka kwa muhula uliopita Alisema, sio suala kwetu tena.

Mchezaji huyo ambaye ni mfungaji bora wa muda wote wa Dortmund katika mashindano makubwa ya Ulaya akiwa na mabao 26.
Hakuna timu katika ligi ya mabingwa ambayo haistahili kuwa kwenye ligi ya mabingwa” Alisema Terzic huku akiongezea kuwa Copenhagen wamerejea kwa mara ya kwanza Champions League toka mwaka 2016.

Dortmund wanashiriki ligi mabingwa barani Ulaya kwa mara ya 20, huku wakiwa wamecheza shindano la vilabu bora la UEFA kila misimu saba iliyopita. Hawajawahi kushindwa na klabu ya Denmark barani Ulaya misimu minne iliyopita, huku Copenhagen wakiwa hawajashinda wapinzani wa Ujerumani katika mecchi kumi.

