VfB Stuttgart Wawatoa Nishai Dortmund kwa Kichapo 5-1!

Borrusia Dortmund wameshindwa kabisa kufurukuta katika mbio za kuuwania ubingwa wa Bundesliga wakiwa nyumbani dhidi ya VfB Stuttgart ambao walipandishwa daraja.

Silas Wamangituka alitangulia kuwaweka kifua mbele Stuttgart baada ya mkwaju wa penati wa dakika ya 26.

Miamba hawa wamejikuta wameshindwa kuzuia kichapo cha aibu cha bao 1-5.

Kichapo hiki kinawafanya mabingwa hawa kusalia katika nafasi ya 5 ya msimamo wa ligi wakiwa nyuma kwa pointi 5 dhidi ya RB Leipzig, ambao walichukua nafasi ya Bayern Munich baada ya kumchapa Werder Bremen bao 2.

VfB Stuttgart Wawatoa Nishai Dortmund kwa Kichapo 5-1!

Bayern pia wanaweza kuwapiku Leipzig ikiwa watapata ushindi dhidi ya Union Berlin Jumamosi ijayo.

Dortmund , ambao walimaliza nafasi ya pili msimu uliopita wamefanikiwa kushinda mechi moja tu ya Ligi ya Bundesliga katika zilizopita, hiki kikiwa ni kichapo chao cha tatu.

Hali imekuwa tofauti sana na matarajio ya wengi, hasa mashabiki wa Dortmund, ambao wanahitaji klabu yao iweze kuwatoa kimaso maso. Dortmund wana kibarua cha ziada kuweka mambo sawa ili waweze kurejea kwenye njia yao ya ushindi.


 

 

MALIZA MWAKA KIBINGWA KWA KUJISHINDIA SHEA YAKO KWENYE SHILINGI 140,000,000TSH!!

Kipindi hiki cha sikukuu kinamalizika kwa namna ya kipekee. Shilingi 140,000,000 kushindaniwa katika michezo ya Evolution kwenye Kasino Mubashara ya Meridanbet. Ingia mchezoni na ujiwekee nafasi ya kushinda shea yako!!!

SOMA ZAIDI

22 Komentara

    Gud news.

    Jibu

    Duuuh niaibu kubwa timu ya Dortmund kufugwa hivyo

    Jibu

    Mpira hautabiriki

    Jibu

    Wametunyima pesa sanaa yani najuta kuwaka kudadadeki

    Jibu

    Ilikuwa aibu ya mwaka kufungwa nyumbani bao 5. Maneno ya wahenga kwamba mpira unadunda ni ya kweli kabisa

    Jibu

    Tatizo mpira hautabiriki

    Jibu

    Good news

    Jibu

    Duh! Aibu

    Jibu

    Da ni noma san

    Jibu

    Duu sio poa

    Jibu

    Ukiangalia utaona jinsi gani mashindano ya UEFA yanazipa wakati mgumu timu zinazocheza mashindano haya, Dortmund wachezaji walikuwa wamechoka baada ya kupindua Meza kwenye mechi ya Uefa kutoka goili moja nyuma adi kuibuka na ushindi.

    Jibu

    Aibu Dortmund wamekuwa wakupiga kama watoto dhuu ishakuwa hatari

    Jibu

    Hongera sana

    Jibu

    Dortmund walipotea

    Jibu

    Hongera zao

    Jibu

    Mpira ni mgumu kutabiri

    Jibu

    Yaani hawa stuttgart wamesababisha kocha kafukuzwa

    Jibu

    Aisee ni noma sana

    Jibu

    Pongezi kwao

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

Acha ujumbe