Mauro Icardi nyota wa klabu ya PSG anakaribia kutua kwa vigogo wa soka nchini Uturuki klabu ya Galatasaray.
Nyota huyo raia wa Argentina inaelezwa ana uwezekano mkubwa wa kuachana na mabingwa haom wa ligi kuu ya Ufaransa baada ya kukaa hapo kwa muda na kushindwa kujihakikishishia namba ya kudumu.
Icardi aliyejiunga na klabu hiyo ya Ufaransa akitokea nchini Italia katika klabu ya Inter Milan amekua na wakati mgumu klabuni hapo chini ya walimu tofauti tofauti wanaopita klabuni hapo ambao wengi wamekua wakimyima muda wa kucheza mshambuliaji huyo.
Kocha wa klabu ya Galatasaray Okan Buruk amedai wako wanapambana kukamilisha dili la mchezaji huyo haraka iwezekanavyo kutoka kwenye klabu ya PSG.
Ni wazi Mauro Icardi anaamua kuondoka klabuni hapo kwenda kutafuta changamoto timu nyingine kwasababu ya ufinyu wa nafasi klabuni hapo.

