Staa wa wa klabu ya Paris Saint German na Mabingwa Watetezi Wa Ligi Kuu Ya Ufaransa Maarufu Kama Legue 1 Klian Mbappe inaelezwa ameingia matatizoni dhidi ya kundi kubwa la wachezaji wa klabu hiyo.
Inadaiwa mkataba mpya ambao staa huyo alisaini mwishoni mwa mwezi Mei na kumfanya kua mchezaji anaelipwa zaidi duniani ulikua na vipengele vya siri ambavyo vinampa mamlaka makubwa mchezaji huyo,kama vile kuwepo kwenye maamuzi ya usajili wa wachezaji vilevile kuamua nani asajiliwe na nani auzwe.
Mkataba huo inaelezwa umevuja na kusababisha hali ya sintonfahamu miongoni mwa wachezaji wa klabu hiyo, kutokufurahishwa na mkataba huo mpya wa Mbappe ikiwemo staa mwenzake Neymar Jr ambae inaelezwa Mbappe alihitaji Neymar auzwe kwenye dirisha la usajili majira haya ya joto na kuzua bifu kubwa baina ya wawili hao.
Wachezaji wengi wa klabu ya PSG inadaiwa hawajapendezwa na kitendo hicho cha mchezaji mwenzao kupewa mkataba ambao unampa mamlaka makubwa zaidi nje uwanja,Pia wachambuzi wengi wameingiwa na wasiwasi huenda hali hii ikaathiri matokeo ya klabu hiyo uwanjani kwani hali hii inaweza kuleta mpasuko mkubwa kwenye timu.
Viongozi wa klabu ya Paris Saint German walilazimika kumpa mkataba wenye thamani na mamlaka makubwa staa huyo wa kifaransa ili kuweza kumshawishi kusalia katika viunga vya Parc De Prince asitimkie kwa miamba ya soka nchini Spain Real Madrid ambayo imekua ikielezwa ni klabu ya ndoto za staa huyo.


