Mshambuliaji wa klabu ya Tottenham Hotspurs na timu ya taifa ya Brazil Richarlison anaelezwa anatarajia kufanyiwa upasuaji katika sehemu zake za siri na inaelezwa kuchukua muda mrefu.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Brazil atafanyiwa upasuaji huo ambapo inaelezwa ni tatizo lililomsumbua kwa muda mrefu, Hivo amekubali kufanyiwa upasuaji ambao utamuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.RicharlisonRicharlison mwenyewe amekiri tatizo hilo limekua likimsumbua kwa muda mrefu lakini hivo amekiri kuzungumza na madaktari na anakwenda kufanyiwa upasuaji kutokana maumivu ambayo amekua akiyapata.

Staa huyo wa kimataifa wa Brazil ambaye amejiunga na klabu ya Tottenham mwaka jana, Amekua hana msimu mzuri sana tangu ajiunge na klabu hiyo kutoka Kaskazini mwa jiji la London.RicharlisonMshambuliaji Richarlison atakua nje ya uwanja kwa kipindi kirefu hivo klabu ya Tottenham itabakua haina mshambuliaji asilia, Ikiwa ni baada ya mshambuliaji Harry Kane kuondoka hivo ni wazi ataacha pengo kipindi ambacho atakua nje ya uwanja.

 JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa