Roy Keane Anamakasiriko Kwa Maguire?

Kwa siku za karibuni, wachambuzi wa soka wamekua kama miungu watu kwenye soka. Roy Keane ni mmoja wao, maneno ndio kazi yao. Kwani anamakasiriko?

Keane anatambulika kama miongoni mwa wachezaji waliokua watukutu uwanjani. Pamoja na yote, aliwahi kuwa nahodha wa Manchester United wakati alipokua mchezaji. Hii inaendana moja kwa moja na ushabiki alionao kwa United.

Roy Keane amekua akitoa maneno ya kila namna kwa baadhi ya wachezaji wa Man United na timu kwa ujumla. Paul Pogba na Harry Maguire ni wachezaji anaowaandama kwa sehemu kubwa.

Hili limetokea tena kwenye mchezo wa Uingereza vs Albania jana usiku. Harry Maguire alipachika goli la kwanza kwa Uingereza na kushangilia kwa namna ya kipekee. Kitendo cha Maguire kushangilia goli lake, kimemkera Keane ambaye ameamua kufunguka vile alivyojisikia.

Kwa mujibu wa Keane, Maguire kushangilia goli kwa kuziba masikio yake ni aibu. Kwa Roy Keane anaona kama Maguire alikua anamaanisha kuwafunga midomo watu wote wanaomkosoa wakati huu ambao amekuwa akiigharimu Manchester United kama mlinzi na nahodha wa timu hiyo.

Maguire hajaliacha hili lipite, mchezaji huyo amejibu mapigo na kudai kuwa, namna yake ya kushangilia hakuielekeza kwa mtu yeyote lakini, anajua wapo watu ambao kazi yao ni kukosoa ma hana tatizo na hilo.


NJIA RAHISI YA MKWANJA NA TITAN DICE

Unawezaje kuikosa hii! njia rahisi ya kutengeneza mkwanja katika kasino maridhawa za meridianbet. Muda wa kufurahia na kutengeneza mkwanja ipo mikononi mwako unasubiri nini?

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.