Sasa ni rasmi, Antonio Rudiger ni mchezaji halali wa Real Madrid kuanzia Juni 1, 2022. Salio la mkataba wake na Chelsea linaisha rasmi wikiendi hii.

Kwa misimu 2 ya hivi karibuni, Rudiger amekuwa muhimili mkubwa kwenye kikosi cha Chelsea. Uwezo wake wa kuiongoza safu ya ulinzi na timu kwa ujumla – ndani na nje ya uwanja, ni vitu vikubwa kwake.

Rudiger

Fununu za kuondoka kwake Stamford Bridge zilizua taharuki, kila mdau akitaka kujua ni kipi hasa kimepelekea sakata la mkataba mpya kutofua dafu na sasa anaondoka kama mchezaji huru? Kila mtu amesema la kwake na sasa, Antonio Rudiger ameweka wazi kilichotokea;

Kwa bahati mbaya, majadiliano ya mkataba wangu yalianza kuwa magumu. Biashara ni biashara lakini, inapotokea hujasikia chochote kutoka kwenye uongozi wa klabu kuanzia Agosti mpaka Januari, hali inabadilika.

Baada ya ofa ya kwanza, kulikuwa na muda mrefu sana uliopita bila taarifa yeyote. Unajua, sisi sio roboti. Hauwezi kusubiri kwa miezi kadhaa bila kujua hatma yako ya mbele.

Ni kweli, hakuna mtu alitarajia vikwazo vingetokea lakini mwisho wa siku, vilabu vingine vikubwa vilionesha uhitaji na, nilipaswa kufanya maamuzi. Nitaishia hapa kwasababu ukiweka biashara pembeni, sina kitu chochote kibaya cha kukisema kuhusu klabu hii.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa