Schmidt: "Sijui Kama Ndio Ilikuwa Mechi ya Mwisho kwa Enzo"

Kocha mkuu wa Benfica Roger Schmidt hana uhakika kama kipigo cha 3-0 hapo jana dhidi ya Braga kilikuwa cha mwisho kwa Enzo Fernandez katika klabu hiyo huku kukiwa na ripoti kwamba amekubali kujiunga na Chelsea.

 

Schmidt: "Sijui Kama Ndio Ilikuwa Mechi ya Mwisho kwa Enzo"

Fernandez aliichezea Argentina wakati wa kampeni yao ya ushindi wa Kombe la Dunia, na kusababisha uvumi wa kuhama wakati wa dirisha la usajili la Januari.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, ambaye alijiunga na Benfica kutoka River Plate mwaka jana, alituzwa kwa juhudi zake kwa kutajwa kuwa Mchezaji Chipukizi wa Mashindano hayo.

Ripoti za Ijumaa zilidai Fernandez alikuwa tayari amekubali kujiunga na The Blues, na mpira sasa uko kwenye uwanja wa Benfica kama wanakubali ofa.

Schmidt: "Sijui Kama Ndio Ilikuwa Mechi ya Mwisho kwa Enzo"

Schmidt; “Sijui kama ilikuwa mechi yake ya mwisho kwa Benfica, ni mchezaji bora, amekuwa akifanya vyema, ametambulishwa na klabu, wakati mwingine mambo hutokea na wachezaji wanapaswa kufanya maamuzi hivyo tutaona kitakachotokea katika wiki zijazo.”

Schmidt alichagua kumwanzisha Fernandez pamoja na Nicolas Otamendi katika mchezo wa jana licha ya mapumziko yao mafupi baada ya ushindi wao wa Kombe la Dunia.

Kocha huyo alaiendelea kusema kuwa Nico na Enzo walikuwa wazuri jana kwani walikuwa katika kiwango chao cha kawaida kama alivyosema kabla ya mchezo, walikuja na mdundo mzuri.

Schmidt: "Sijui Kama Ndio Ilikuwa Mechi ya Mwisho kwa Enzo"

Wengine walikuwa kwenye Kombe la Dunia, hawakucheza, hawakufanya mazoezi mengi. Wanahitaji muda kurejea katika hali yao bora. Kwa ujumla hawakuwa wazuri vya kutosha na hawawezi kubadilika.

Acha ujumbe