Klabu ya Simba SC itajitupa uwanjani tena leo kuvaana na Costal Union kutoka Tanga katika uwanja wa Benjamin Mkapa Stadium majira la saa moja jioni kwa muda wa Afrika Mashariki.
Simba SC inarejea tena katika Ligi ya kuu ya NPL kwaajili ya kutetea ubingwa wao, baada ya kupata ushindi mwembamba wa goli 1-0 dhidi ya Polisi katikati ya wiki.
Kocha msaidizi wa Simba SC, Seleman Matola amesema mapungufu yaliyojitokeza kwenye mechi zilizopita kama kutengeneza nafasi na kushindwa kuzitumia vizuri yameendelea kufanyiwa kazi na anaamini tutapata ushindi mnono.
“Ni kweli tumekuwa hatupati ushindi mnono lakini tumeyaona mapungufu yetu na tumeyafanyia kazi, matumaini yetu ushindi mnono utaanza kupatikana tukianza katika mchezo wa leo,” amesema Matola.
Simba SC inatendelea kuwakosa wachezaji wake, Chris Mugalu ambaye anaendelea kupona taratibu, wakati Taddeo Lwanga na Pape Ousmane Sakho wakiwa wamepona lakini hawako fiti asilimia 100 kuwepo katika kikosi.
JIUNGE KWENYE SHINDANO LETU LA EXPANSE NA USHINDE!
Achana na ndoto za usingizini za kuokota burungutu la pesa, amkia upande wa ushindi halisi kutoka Meridanbet kwenye shindano la Expanse linalojumuisha michezo pendwa ya sloti za mtandaoni iliyopo kwenye promosheni ya Expanse kutoka Meridianbet.