Klabu ya Simba SC imeshindwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuondolewa kwa penati 4-3 katika mchezo wa Robo Fainali dhidi ya Orlando Pirates uliochezwa kwenye Uwanja wa Orlando Nchini Afrika Kusini.
Katika dakika 90 za kawaida Orlando ilishinda goli 1-0 hivyo matokeo ya jumla kuwa 1-1 kwani Simba ilipata ushindi wa goli 1-0 katika mchezo wa awali katika hatua hiyo.
Mshambuliaji Chris Mugalu alipata kadi nyekundu katika dakika ya 58 na kufanya mchezo huo kuwa mgumu zaidi kwa wageni Simba SC lakini waliweza kumudu na kufikia hatua ya matuta.
Penati za Simba katika mchezo huo ambao zilifungwa na Shomari Kapombe, Meddie Kagere na Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ wakati Jonas Mkude, Enock Inonga wakikosa.
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.